Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Linus Nyoni mkazi wa Mbagala, Charambe jijini Dar es salaam amepigwa risasi na polisi baada ya kujaribu kutaka kuwakimbia askari polisi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 30, 2018. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa mtu huyo alikamatwa Mnamo Machi 16, 2018 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya unyang’anyi kwa kutumia silaha katika maeneo ya Mbagala na Mkuranga.
Mambosasa amesema kuwa Askari polisi walivyoenda kupekua nyumbani kwa mtuhumiwa huyo walikuta bastola moja aina ya Browing ambayo hata hivyo ilikuwa imefutwa namba.