Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlinzi wa shule auawa, wauwaji wabeba kichwa

Mlinzi Pic Data Matukio yakikatili yamekua yakishika kasi nchini.

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

 Mwili wa mlinzi huyo umekutwa leo Jumatano Februari 2, 2022 asubuhi na wafanyakazi wa shule hiyo inayomilikiwa na Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meya Iranghe amesema alipata taarifa za kifo cha mfanyakazi wake mmoja leo asubuhi na baada ya kufika eneo la tukio aliwakuta Polisi.

Iranghe amesema bado chanzo na waliofanya mauaji haya hawajajulikana.

"Naomba kuwasiliana na Polisi ambao ndio wanaendelea na uchunguzi wa tukio hili mimi nimepigiwa simu na wafanyakazi na nimekuta tayari polisi wapo hapa" amesema

Maofisa wa Jeshi la Polisi waliokuwa katika eneo la tukio wameeleza taarifa rasmi itatolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

"Ni kweli tukio limetokea lakini msemaji ni Kamanda wa Polisi Mkoa atatoa taarifa rasmi "amesema mmoja wa maofisa wa Jeshi hilo ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Mary Kupesha hakupatikana kutoa taarifa ya tukio hilo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz