Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlinzi auawa kwa kucharangwa mapanga

Mauaji Mlinzi auawa

Sat, 18 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali ya kusikitisha mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Said Kabona ambae alikuwa mlinzi katika kampuni ya Nasri Block amekutwa ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu ambao bado hawajafaamika katika eneo la Nguvukazi Chanika Jijini Dar es salaam hali iliyozua sintofahamu kwa wakazi wa eneo hilo.

Akizungumzia tukio hilo, wenyekiti wa eneo hilo Barnabas Mtumbuka ambae ameeleza namna alivyopata taarifa za tukio hilo ambapo alipigiwa simu usiku wa manane kuhusiana na tukio hilo.

Aidha Mtumbuka akaeleza namna alivyopigiwa simu usiku wa manane baada ya marehemu kukutwa katika mazingira tofauti na alipokuwa akifanyia kazi ya ulinzi.

Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo akatoa rai kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata sheria na taratibu za nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live