Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlinzi auawa akiwa kazini

PANGA Ed Mlinzi auawa akiwa kazini

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu ambao hawakufahamika kwa haraka majina yao, wamevamia na kuvunja duka katika Mtaa wa Mwananchi, Manispaa ya Ilemela, mkoani hapa na kuiba vitu mbalimbali kisha kumuua mlinzi aliyekuwa lindoni.

Mlinzi huyo ameuawa kwa kushambuliwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mmoja wa wamiliki wa duka hilo, Isack William, alisema alipofika dukani huko majira ya asubuhi, walikuta makufuri yamekatwa na taa zimenyofolewa na alipofungua mlango na kuingia ndani, alibaini bidhaa zimechukuliwa na mlinzi akiwa amelala huku kichwa chake kikivuja damu.

William alisema kuwa baada ya kushuhudia hilo, alimwita jirani yake ili amwangalie kama wanaweza kumpeleka hospitalini, lakini baada ya jirani huyo kufika walibaini alikuwa amefariki dunia, ndipo wakatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Kata ya Buzuruga, Catherine Thomas, alitaja hatua zinazoendelea kuchukuliwa za kuhamasisha na kusimamia suala la ulinzi na usalama katika mtaa huo ili kudhibiti uhalifu wa namna hiyo.

"Tayari tumeitisha kikao cha dharula ili tuone sasa ni kwa namna gani tunaanza na hili jambo, kwa maana tangu nimeingia katika uongozi ni tukio la kwanza kutokea," alisema Catherine.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gideon Msuya, alisema tayari jeshi hilo limeanza uchunguzi ili kubaini wahusika wa uhalifu huo.

Msuya alitoa rai kwa wafanyabiashara wote mkoani humo kuajiri walinzi ambao wamepitia mafunzo na ambao wana uwezo wa kujihami ili kukabiliana na wahalifu wa namna hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live