Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi wa Mashitaka atua Babati, afuta kesi 51

679a812e258e0c92b27b8e1f4d59f2c9 Mkurugenzi wa Mashitaka atua Babati, afuta kesi 51

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amefuta kesi za watuhumiwa 51 wakiwamo wanaume 49 na wanawake wawili waliokuwa wakikabiliwa na makosa mbal- imbali katika gereza la Babati mkoani Manyara na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani.

Amewasisitiza mawakili wa Serikali kuendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha watu wanao- fanya makosa wanaendelea kubaki gerezani na wale walioonewa wanawatoa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake ya kukagua shughuli za mashitaka mkoani hapa, Maganga alisema miongoni mwa watuhumiwa hao 51 , yupo mzee wa miaka 85 ambaye alikuwa anak- abiliwa na shitaka la kubaka.

Mganga ambaye alitembelea gereza la Babati akiongozana na viongozi mbalimbali kutoka ofisi ya taifa ya mashitaka, alisema alifanya ziara hiyo na wadau kusikiliza na kufahamu changamoto za kwenye magereza na kuzitafutia ufumbuzi.

‘’Nimeweza kusikiliza ma- tatizo yao nikawafutia kesi za makosa madogo watuhumiwa 51 na hilo ndilo nililoanza nalo hivyo nitaendelea na shughuli zingine ndani ya ofisi na kutembelea wadau kuona ushirikiano ukoje wanajipanga kuhakikisha kwamba shughuli za mashtaka nchini zinaenda kama kawaida”, alisema. Alifafanua kwamba wale walio-

achiwa huru walikuwa wanakabili- wa na mashitaka madogo na baadhi wakiwa wazee walikuwa wanak- abiliwa na kesi ya mauaji ambapo baada ya kuangalia aligundua kuna shida na hivyo kuwaachia huru.

Alieleza kuwa kulikuwa na mzee wa miaka 85 aliyekuwa akik- abiliwa na kesi ya kubaka ambapo baada ya kubaini kuwa kulikuwa na sintofahamu ikabidi afanye uamuzi kumuachia huru.

Aidha DPP alisema kesi zote za dawa za kulevya zimebaki kwani serikali haiwezi kujenga taifa la watu wanaojihusisha na dawa pamoja na nyara za serikali hivyo aliamuru wabaki.

‘’Nimekutana na wale ambao waliua pundamilia kumi na kitu kwa kuwachoma mikuki, nime- amuru wabaki hata kama ni watoto wadogo, kuna mmoja ana miaka 15 yeye nimeamuru atoke manake ni mtoto lakini mkubwa wa miaka 25 abaki ili wajifunze jinsi ya kulinda mali asili zetu”, alisema.

Alisisitiza, ‘’Kwa ujumla tu- naenda vizuri na kesi zinaendelea vizuri na watu wanatiwa hatiani, hata jana kuna mama amefungwa miaka 30 kwa kosa la kukutwa na mirungi, sasa watu wajifunze.”

“Na sisi tunaendelea kuwasisiti- za mawakili wa Serikali kuendelea kushirikiana na wadau ili kwa wale wote ambao wamefanya makosa tuwe nao lakini ambao wameone- wa tuwatoe, ndicho tunachotaka kufanya.’’

Kamishina msaidizi wa Mag- ereza, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara,Prosper Kinyaga alisema ujio wa DPP ni muhimu kwa sababu watu 51 walioachiwa huru wamepunguza msongamano hivyo una manufaa kwao na ume- punguza gharama za kulisha na kuhudumia.

‘’Ujio wake umetusaidia kwani umetupunguzia karibia zero moja na pia umepunguza kazi ya ku- walisha huku wakiwa hawafanyi kazi yoyote na pia imeipunguzia serikali gharama ya kuwahudumia. Kama tutaendelea hivi manake tunapunguza msongamano magereza yetu kwa sababu bado ni madogokwa maana ya uwezo wa kuchukua watu wengi kwa mara moja,’’ alisema .

Chanzo: habarileo.co.tz