Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi kortini utakatishaji mil 360.8/-

21bc284057765ba755e5575cfe684f8a.jpeg Mkurugenzi kortini utakatishaji mil 360.8/-

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKURUGENZI wa kampuni ya Barmat Intenational Mining Company Limited, Badru Amrani, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu

Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kusomewa mashitaka matano likiwemo la kutakatisha fedha haramu zaidi ya Sh milioni 360.8.

Amrani alifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serika-li Mwandamizi, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu. Katika shitaka la kwanza, Wakili Wankyo alidai kuwa, Amran anadaiwa kughushi nyaraka.

Ilidaiwa mahakamani kuwa, Desemba 6, 2019 katika Mkoa wa Dar es Salaam, mshitakiwa alighushi ripoti ya maabara ya mkemia wa madini akionesha ni ripoti halali iliyotolewa na Africa Mineral And Geosciences Center (AMGC) kuthibitisha kuwa madini ya ‘manganise’ yalijaribiwa na kuthibitishwa kuwa na kiwango cha asilimia 47.78.

Aliendelea kudai kuwa katika shitaka lingine, Februari 16, 2020 mshitakiwa huyo aligushi nyaraka za mauziano ya madini ya shaba kati ya kampuni yake na kampuni ya BTC General Trade FZE Company Limited kutoka Falme za Kiarabu kwa makubaliano kuwa, angeipelekea kampuni hiyo tani 1000 za madini hayohuku akijua si kweli.

Wakili Wankyo alidai pia kuwa, kati ya Novemba 23, 2020 na Desemba 21, 2020 katika Mkoa wa Dar es Salam, mshitakiwa huyo alijipatia Sh 360,847,995 kutoka kwa Kerim Mankeyev, Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya BTC General Trade FZE Company Limited baada ya kudanganya kwamba angewapelekea tani 1000 za shaba huku akijua ni udanganyifu.

Katika shitaka lingine ilidaiwa kwamba, Machi 23 mwaka 2021, eneo la Bunju, Kinondoni Dar es Salaam, mshitakiwa alikutwa akimiliki madini yenye thamani ya Sh 577,987.56 bila kuwa na leseni ya kufanya biashara ya madini.

Katika shitaka la mwisho, Wakili Wankyo alidai kati ya Novemba 23, 2020 hadi Desemba 21, 2021 mshitakiwa alitakatisha Sh 360,847, 995 huku akijua ni zao la makosa tangulizi ya kugushi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz