Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi Vodacom, wenzake 8 kizimbani

50499 VODA+PIC

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hisham Hendi na wenzake wanane wamefikishwa kortini kwa tuhuma 10.

Akiwasomea hati ya mashtaka jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakili wa Serikali Jackline Nyantori akisaidiwa na Wankyo Simon mbele ya hakimu mkazi mkuu, Huruma Shaidi alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 20/2019.

Katika mashtaka hayo 10; yapo ya kuingiza, kutumia na kusimika vifaa vya mawasiliano kinyume na sheria, kugawa namba za masafa bila kuwa na leseni, kumiliki vifaa kilaghai pamoja na mashtaka mawili ya kuisababishia Serikali hasara.

Mbali na Hendi, washtakiwa wengine ni meneja uendeshaji wa biashara wa kampuni ya Inventure Mobile Tanzania, Ahmed Ngassa, mtalaamu wa Tehama ambaye ni raia wa Kenya, Brian Lusilola. Kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd/A Tala Tanzania. Wengine ni mkuu wa idara ya mapato wa Vodacom, Joseph Nderitu; mkurugenzi wa huduma za sheria wa Vodacom, Olaf Mumburi na mkuu wa idara ya mauzo wa Vodacom, Joseph Muhere, meneja wa fedha wa Vodacom, Ibrahim Bonzo na kampuni ya Vodacom yenyewe.

Katika kosa la kuingiza vifaa nchini, wanaoshtakiwa ni Ngassa, Lusiola na kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd / A Tala Tanzania.

Wanadaiwa kuingiza vifaa vya mawasiliano aina ya Proliant ML1 Gen 9 Server (Pabx Virtual Machine) kinyume cha sheria.

Katika shtaka la saba, Ngassa, Lusiola na kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd/ A Tala Tanzania wanashtakiwa kumiliki vifaa kilaghai na kutumia namba ya simu bila kuthibitishwa na TCRA kwa nia ya kukwepa gharama na kuruhusu mawasiliano ya kimataifa kuingia nchini.

Katika shtaka la tisa, Hendi, Nderitu, Mumburi, Muhere na Bonzo wanadaiwa kutumia kifaa cha mawasiliano ambacho hakijasajiliwa nchini wala kupata idhini kutoka TCRA na la 10, ni Hendi, Nderitu, Mumburi, Muhere na Bonzo kuisababishia TCRA na Serikali hasara ya Sh5.25 bilioni.

Hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza kesi inayowakabili hivyo kuwekwa rumande hadi April 17 itakapotajwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz