Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media atiwa hatiani

8c1dcdee2158b637aefcc0318ad054a0 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media atiwa hatiani

Wed, 18 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha nje Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuzuia askari kutekeleza majukumu yao, kwa masharti ya kutokurudia kosa hilo ndani ya mwaka mmoja.

Hukumu hiyo ilisomwa mahakamani hapo jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Faraji Ngukah.

Pia mahakama hiyo imemwachia huru mshtakiwa namba mbili katika kesi hiyo, Mike Mushi baada ya kukuta hana hatia katika makosa yote yaliyokuwa yakiwakabili ambapo hakimu Shaidi alisema Mushi alikuwa ni kama msindikizaji katika kesi hiyo.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao kwa kuleta mashahidi sita huku Melo akijitetea mwenyewe bila kuwa na shahidi mwingine.

Awali kabla ya kusomwa hukumu hiyo, Wakili Ngukah aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwani kitendo alichokifanya cha kuzuia askari kutekeleza majukumu yao ni hatari kwa taifa.

Akimtetea mteja wake wakili wa utetezi, Bernedict Ishabakaki aliomba kama sheria inatoa nafasi ya faini mahakama imehukumu kutoa faini kwani ana vijana ambao amewaajiri na wanamtegemea hivyo faini itakuwa fundisho.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Shaidi alisema mshtakiwa alionekana kuwa na makosa katika kesi ambazo zilifunguliwa awali ambazo zote zilikuwa na makosa yanayofanana.

"Jeshi la Polisi liko kwa ajili yetu sote kazi yake ni kupeleleza na sisi ni wajibu wetu kushirikiana nalo na mahakama inaweza kukumbusha hilo," alisema hakimu Shaidi na baadaye akasoma hukumu hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz