Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkunga atenganisha kichwa na kiwiliwili cha mtoto mama akijifungua

98017 Uganda+pic Mkunga atenganisha kichwa na kiwiliwili cha mtoto mama akijifungua

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Uganda. Polisi nchini Uganda, wanachunguza taarifa za mkunga ambaye anadaiwa kushindwa kumhudumia mjamzito na kusababisha mtoto kutengana kichwa na kiwiliwili wakati mama huyo akiwa anajifungua.

Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti mkasa huo uliotokea mjini Busia likisema mama huyo alikuwa akijifungua na kichwa cha mtoto huyo kilitengana na kiwiliwili

Gazeti hilo limemnukuu mama huyo, Lilian Musazi akidai kuwa muuguzi huyo alimvuta mtoto huyo miguu ambayo ndio ilianza kutoka.

Familia ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21 imesema mama huyo alipoingia kwenye chumba cha kujifungulia alisubiri sana kabla ya kuhudumiwa.

Lilian amekuwapo katika kituo cha afya cha Bulumbi nchini humo kwa siku nne akisubiri muda wa kujifungua ufike.

Imeelezwa kuwa baadaye familia yake iliwasilisha ombi la kutaka kumhamisha mama huyo kwenye hospitali nyingine kama wangekuwa wametambua kuwa kuna tatizo.

Pia Soma

Advertisement
Kituo hicho cha afya kina wakunga wawili ambapo mmoja pekee anakuwepo zamu kwa wiki moja.

Wakati mkunga huyo anamhudumia mjamzito huyo alikuta miguu ishaanza kutoka huku mwili ukiwa umekwama kwenye mabega.

 “Alimvuta mtoto na baadaye akaenda kukaa. Baada ya muda akarudi akaniambia nimsukume lakini mtoto alikataa kutoka. Alianza kumvuta na kumgeuzageuza, nililia sana akaniambia kama nataka niondoke . Nawezaje kuondoka wakati mtoto ametoka nusu,” amenukuliwa mama huyo na gazeti hilo.

Mama huyo anasema mtoto wake alikuwa mzima kutokana na ushahidi wa miguu yake iliokuwa ikicheza.

Taarifa zinasema kuwa tukio hilo limezua hisia nchi Uganda wananchi wakitoa wito kwa Serikali kuwapa mafunzo wakunga jinsi ya kusaidia kujifungua.

Mwenyekiti wa kijiji, Ibrahim Okello ameiomba serikali kuwaabadilisha wakunga kwenye kituo hicho cha afya.

Chanzo: mwananchi.co.tz