Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude atupwa jela maisha kwa udhalilishaji

Kufungwa Ms Mkude atupwa jela maisha kwa udhalilishaji

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Iringa imemhukumu mkazi mmoja wa wilaya.hiyo kifungo cha maisha jela na kulipa fidia ya shilingi milioni tano baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumdhalilisha mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka 11.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Said Mkasiwa amesema mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili dhidi ya mshtakiwa Mkude Nziku mwenye umri wa miaka 20.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Mkude ambaye ni baba mdogo wa mtoto aliyefanyiwa ukatili alitenda unyama huo mwezi Novemba mwaka 2023 katika kijiji cha Kihanga wilayani Iringa.

Imeelezwa siku ya tukio mtuhumiwa aliingia chumbani kwa binti huyo kupitia njia ya dirishani akamchukua mtoto huyo kwa nguvu kutoka kitandani akamuweka chini na kumvua nguo, kisha kutenda unyama huo.

Kesi hii ilikuwa na mashahidi wanne akiwemo (Mtoto mwenyewe aliyetendwa, mama Mzazi, Daktari pamoja na Polisi aliyechukuwa maelezo ya awali)

Shahidi wa pili ambaye ni Mama Mzazi wa mtoto huyo anasema baada ya kusikia kelele za mwanae alitoka haraka hadi chumbani kwa mwanaye akapishana na mtuhumiwa sebuleni na alianza kumkimbiza Mkude akaanguka chini na mama akammulika na taa yake ya Solar na kumtambua kuwa ni yeye na akamuuliza ulikuwa unafanya nini chumbani kwa binti yako (Mtoto wa kaka yako) Mkude akadai kuwa alikosea nyumba kisha akakimbia.

Mama huyo anaendelea kusimulia kuwa alivyorudi chumbani akamkuta mtoto wake akilia kwa maumivu makali na alivyomkagua akaona akitokwa na damu sehemu za Siri.

"Alinivua sketi akaivuta nguo yangu ya ndani akaniingiza 'LIDUDE' lake sehemu ya kukojolea nilihisi maumivu makali nikapiga kelele mama akaja chumbani kwangu, lakini Mkude akakimbia," alisema mtoto huyo.

"Nilimchukua Mwanangu hadi ofisi za kijiji kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana walimshauri mtoto asioge hadi asubuhi ili aende hospitali kupimwa.

Ushahidi kutoka kwa shahidi wa tatu unaeleza alimpokea mtoto huyo akiwa na michubuko, damu huku akiwa hana usichana wake kitendo kinachoashilia aliingiliwa.

Uchunguzi wa daktari umebaini kuwepo kwa michubuko sehemu za siri za mtoto huyo, hali iliyosaidia ushaidi. Hakimu Mkasiwa amesema mahakama imetoaadhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.

Hata hivyo kabla ya hukumu kutolewa Mtuhumiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo alisema siku ya Novemba 16 alikuwa akijiandaa kwenda shambani akakamatwa na migambo na alipohoji akaambiwa anatuhumiwa kwa kesi ya kubaka ila aliomba Mahakama imuachie huru ili akaendelee kuwalea wazee na kuwasomesha watoto maana yeye ndiyo tegemezi na wazazi wake umri umekwenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live