Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkojo wa sungura watumika kufukuza wadudu

SUNGURA Mkojo wa sungura watumika kufukuza wadudu

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na mfumo wa ulaji kubadilika na watu kupenda kula Chakula cha asili, Chuo Kikuu Mzumbe kimekuja na ubunifu wa mkojo wa Sungura kwa kilimo Cha matunda na mbogamboga.

Katika kufanya tafiti zake,Chuo kimegundua kuwa mkojo wa Sungura unaharufu kali hivyo sio rafiki kwa wadudu hasa wale waharibifu katika mboga zenye jamii ya maua na matunda.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba,Mwanafunzi wa Sayansi ya Uzamili Chuo Kikuu cha Mzumbe, Nelson Kissanga amesema kuja na mfumo huo kwa wakulima wameunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ni mahali sahihi ya Biashara na Uwekezaji.

Amesema Chuo chao pia kinandaa wataalamu kwa kauli mbiu ya kujifunza kwa maendeleo ya watu.

"Tumekuja na ubunifu huu ambao utasaidia wakulima kutopata hasara pindi wadudu watakapoingia katika bustani na kuharibu mbogamboga na matunda,”amesema na kuongeza.

"Wadudu ni waharibifu katika mbogamboga na mboga zenye jamii ya maua pamoja na matunda kwani wanapenda kuvutiwa sana na mvuto wake katika kufata harufu nzuri ya maua hasa yanapochanua,”amesema Kissanga.

Amesema Mkojo wa sungura ni mbadala wa utumiaji wa kupuliza madawa katika mbogamboga na matunda ambapo yanakuwa na madhara kwa watu wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live