Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkoa wa Manyara ni wapili kitaifa kwa matukio ya ukatili wa kijinsia

Kuzagaza Kuzaga ameongea na viongozi na wananchi ili kupunguza matukio hayo

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga amewataka wananchi na viongozi wa eneo hilo kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo yamekithiri Manyara.

Kamanda Kuzaga ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, viongozi wa dini na wazee maarufu wa mji huo.

Amesema mkoa wa Manyara ni wapili kitaifa kwa matukio ya ukatili wa kijinsia hivyo jamii inapaswa kushirikiana ili kutatua tatizo hilo ambalo limekithiri.

“Hata mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere huwa anasema tupambane tuondokane na ukatili tubaki kuongoza kwenye kukusanya mapato na mengineyo siyo ukatili wa kijinsia kwani tumezidisha,” amesema Kamanda Kuzaga.

Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani, Adam Justin Kobelo ametoa ombi kwa kamanda Kuzaga kuongeza magari mawili kwa ajili ya askari wa kituo cha polisi Mirerani.

“Polisi wa Mirerani wanahudumia tarafa nzima ya Moipo na zaidi hivyo kuwa na gari moja au mawili hawawezi kutenda kazi zao ipasavyo,” amesema Kobelo.

Mjumbe wa mamlaka ya mji huo Claudia Dengesi amesema jamii inapaswa kushirikiana na dawati la jinsia la polisi ili kuhakikisha wanatokomeza ukatili wa kijinsia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live