Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Mkesha’ mahakamani

28725 Pic+mkesha TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (Wetcu Ltd), Ijumaa ilikilizwa hadi saa 3:00 usiku huku wakili wa utetezi akijitoa kupinga alichodai vitisho dhidi ya wateja wake kutoka serikalini.

Uamuzi huo ulilenga kuwapa fursa washtakiwa wote kutoa utetezi kabla ya shauri kuahirishwa hadi Desemba 10.

Kabla shauri hilo kuahirishwa, wakili Chombala Kanani anayewatetea washtakiwa alijitoa dakika za mwisho baada ya wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuileza mahakama kuwa Serikali inakusudia kuwachukulia hatua watu wanaodaiwa kuingiza baadhi ya nyaraka gerezani bila kuzingatia mahitaji ya kisheria. Hata hivyo, hakuzifafanua.

Kimaro alidai Serikali haiwezi kuchezewa kiasi hicho na itabidi wahusika wakamatwe kuhojiwa.

Kauli hiyo ilitolewa baada ya mshtakiwa wa saba, Faraz Abbas kuiomba mahakama ipokee nyaraka kutoka kampuni ya Toyota Tanzania ili iwe sehemu ya ushahidi wake ombi ambalo lilipingwa na Kimaro kuwa, iliingizwa gerezani kinyemela bila kufuata taratibu.

Kufuati hali hiyo, Kanani aliinuka na kumweleza hakimu Chiganga Mashauri kuwa hataendelea kutokana na vitisho vya Serikali.

Washtakiwa wengine aliyekuwa mwenyekiti wa Wetcu Ltd, Gabriel Mkandala; makamu wake, Msafiri Said; kaimu meneja, John Kusaja; mhasibu mkuu, Prosper Mbacho; Hamza Kapera na Fransis Penta.

Wote wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi.

ambayo ni Kula njama, Kughushi, Matumizi mabaya ya ofisi, Kufanya manunuzi bila kibali na Kuisababishia hasara mamlaka ya Serikali, makosa ambayo inadaiwa waliyatenda kati ya Juni mosi hadi Julai 31 mwaka 2015.



Chanzo: mwananchi.co.tz