Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya na wanaye wawili wauawa na mumewe Marekani

Njoki Missed Red Flag 1.png Mkenya na wanaye wawili wauawa na mumewe Marekani

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Marekani wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja Mkenya aliuawa pamoja na watoto wake wawili na baadaye mume wake akajitoa uhai katika mtaa wa Valley Station, jijini Louisville.

Mwanamke huyo aliyetambulishwa kama Njoki Muchemi Stanton, mwenye umri wa miaka 49, alipatikana amekufa kando ya mumewe, Gary Stanton mwenye umri wa miaka 60. Wote walikuwa na majeraha ya risasi.

Mabinti wake, Muchemi Andrianna Stanton mwenye umri wa miaka 17 na Brianna Stanton mwenye umri wa miaka 11, pia walipatikana wakiwa wameaga dunia.

Polisi wametaja kisa hicho kuwa mauaji ya kinyumbani, wakisema waathiriwa wote walikuwa wa familia moja.

Huku uchunguzi zaidi wa Kitengo cha Mauaji cha LMPD ukiendelea, inaripotiwa kuwa mwanamume huyo ndiye aliyetekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Maelezo kwenye ukurasa wa Facebook wa marehemu Njoki yanadokeza kwamba alikuwa amesherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi majuzi ambapo mumewe Gary alimtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live