Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya, Mkongo mbaroni kwa kutapeli milioni 9

MBARONI.jpeg Mkenya, Mkongo mbaroni kwa kutapeli milioni 9

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo wakikabiliwa na mashitaka ya kujipatia Sh milioni tisa kwa njia ya udanganyifu. Washitakiwa hao ni Kasongo Kyungu (38) mkazi wa Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sebby Ndong (30) mkazi wa Lio, Kenya.

Akiwasomea hati ya mashitaka, askari Maida Kimanzi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Claudius Kipande alidai kuwa Mei 20, mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku katika Mtaa wa Samora, Kata ya Kivukoni mkoani Dar es Salaam walijipatia Sh milioni tisa mali ya Macao Kasino kwa kudanganya kuwa wameshinda katika mchezo wa kubahatisha jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Washitakiwa wote walikana mashitaka yao. Mlalamikaji Nancy Marro alidai kuwa anatarajia kuwa na mashahidi kadhaa na kielelezo cha mkanda wa video. Washitakiwa walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini fungu la dhamana la Sh 500,000 kwa kila mdhamini.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live