Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke asimulia mumewe aliyetekwa Dar alivyopatikana Kenya

65363 Pic+mke

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Veronika Kundya, mke wa mfanyabiashara mwenye asili ya Kenya, Raphael Ongangi amesema mumewe aliachiwa na watekaji karibu na duka la shangazi yake mjini Mombasa , Kenya.

Ongangi alitekwa Oysterbay jijini Dar es Salaam Juni 24, 2019 na kupatikana jana Julai  2, 2019 huko Kenya.

KWa mujibu wa Veronika, mumewe hajui alifikaje eneo hilo ila ajikuta yupo jirani na duka hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Julai 3, 2019

Veronika amesema kwa sasa hawataki kufahamu mengi zaidi ya kumshukuru Mungu baada ya mumewe kupatikana akiwa hai.

“Kikubwa ni kwamba yupo salama, hana majeraha na amesema hakupigwa ila hajui alifikaje karibu na duka hilo la shangazi yake.”

Pia Soma

“Leo tulikwenda hospitali kwa ajili ya vipimo vya kawaida nashukuru yuko vizuri hana shida na muda huu amepumzika,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz