Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke amtuhumu mumewe kumjeruhi kwa kukataa kuingiliwa kinyume na maumbile

41895 KISAMVU+PIC Mke amtuhumu mumewe kumjeruhi kwa kukataa kuingiliwa kinyume na maumbile

Fri, 15 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Mwanamke mmoja mkazi wa Kijichi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, anadai kupigwa na kujeruhiwa usoni ambako ameshonwa nyuzi sita na mumewe baada ya kumkatalia kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Akizungumza leo Alhamisi Februari 14, 2019 mwanamke huyo anadai mume wake  amekuwa akimtaka wafanye mapenzi kinyume na maumbile muda mrefu lakini amekuwa akikataa kwa sababu ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya dini.

Akieleza zaidi alidai kwa muda mrefu ndoa yake imeingia kwenye mgogoro na mumewe amekuwa akimwambia kuwa hajui mapenzi.

“Alianza kunitaka kinyume na maumbile miezi mitatu tangu anioe nikamkatalia, mpaka nikapata mimba ikiwa na miezi sababu bado akawa anataka nikamkatalia,” anasema.

Amedai kuwa baada ya kufuatlia historia ya mumuwe, majirani wanaomfahamu walimweleza kuwa tabia hiyo ndiyo imesababisha kuachana na wake zake zaidi ya wawili.

Hata hivyo, mwanaume huyo amekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa mgogoro wa ndoa yake umesababishwa na wakwe zake wanaomdai mahari mpaka imefikia hatua ya kumweleza kuwa ni maskini.



Chanzo: mwananchi.co.tz