Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke amcharanga mumewe sehemu za siri kwa wembe

Matibabu Makubwaaa.png Mke amcharanga mumewe sehemu za siri kwa wembe

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri (Korodani ya kushoto) mumewe Vintan Luhiva (42).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Joseph Konyo amesema mtuhumiwa aliweza kufanya tukio hilo wakati mwanaume huyo akiwa amesinzia huku chanzo kikiwa hakijabainishwa.

Ameeleza kuwa mtuhumiwa alichukua wembe na kumjeruhi kwa kumkata korodani moja upande wa kushoto na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda Konyo amesema majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Tunduru akipatiwa matibabu na kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kutenda tukio hilo yupo mikononi mwa Polisi na hatua za kumpeleka Mahakamani zinafuata baada ya hatua za upelelezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live