Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke ajiua baada ya mume kumuua mchepuko wake

Panga WATU wawili wamekufa akiwemo kijana aliyeuawa kwa panga baada ya kufumaniwa.

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: Habarileo

WATU wawili wamekufa akiwemo kijana aliyeuawa kwa panga baada ya kufumaniwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema jana kuwa mwanamke aliyefumaniwa na kijana huyo alijiua kwa sumu.

Kamanda Maigwa alisema mjini Moshi kuwa, Anna Shirima (26) na Juvenal Peter (23) walifumaniwa Desemba 4 mwaka huu saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Kibaoni, Kata ya Nanjara wilayani Rombo katika mkoa huo.

"Baada ya fumanizi mwanaume alicharangwa mapanga na mume wa dada huyo hadi kifo lakini mwanamke kutokana na fedheha ya tukio hilo naye alikunywa sumu na alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Huruma Rombo," alisema.

Kamanda Maigwa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa awali mume wa Anna, Riziki Shirima (26) alichukua simu ya mkewe akakuta ujumbe mfupi wa kimapenzi baina ya mkewe na Peter.

Alisema Shirima alimuwekea mtego Peter akafanikiwa kumnasa na akamkatakata kwa panga hivyo kusababisha kifo cha kijana huyo.

Kamanda Maigwa alisema baada ya tukio hilo Shirima alijisalimisha katika kituo cha Polisi Rombo na bado yupo rumande kwa ajili ya hatua za kisheria.

Chanzo: Habarileo