Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke aeleza ujasiri alioonyesha mumewe baada ya kufukua mguu

57291 Pic+mauaji

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbarali. Mama wa mtoto anayedaiwa kuuzwa na baba yake na baadaye kuuawa na kunyofolewa viungo amesimulia jinsi mumewe alivyoonekana jasiri baada ya kuuona mguu aliosema ni wa mwanaye kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi.

Mtoto huyo, Rose Nguku (6), ambaye aliuawa kwa kunyongwa, alikuwa akiishi na baba yake, Japhet Nguku maeneo ya Igurusi wilayani Mbarali. Baba huyo anatuhumiwa kumuuza mwanaye kwa mfanyabiashara anayeitwa Andrew Mwambuluma. Polisi inawashikilia wawili hao kwa tuhuma za mauaji.

Jana, Scola Chafumbwe, ambaye ni mama wa mtoto huyo, pia mkazi wa Igurusi, aliiambia Mwananchi akiwa nyumbani kwa wakwe zake, kuwa walishangazwa na jinsi mumewe alivyokuwa jasiri wakati alipofukua mfuko uliokuwa na mguiu wa mwanae.

Alisema alitengana naye na kurudi kwao mkoani Njombe kutokana na kipigo, akiwaacha watoto wao watatu kwa mzazi mwenzake.

“Nimeishi naye miaka 12. Maisha yangu yote yamekuwa ya kipigo siku zote,” alisema Scola.

Lakini alisema alirudi baada ya kupona kabla ya kuondoka tena kwenda Njombe baada ya kifo cha mama yake mzazi.

Habari zinazohusiana na hii

Baadaye alipigiwa simu kuwa binti yao amepotea na alipowasiliana na mumewe, ambaye alithibitishiwa habari hizo ndipo alipoamua kwenda Mbalizi ambako walianza kumsaka binti huyo bila ya mafanikio na hivyo kukubaliana kurudi nyumbani kwa mkwe wake ili kuzungumzia suala hilo.

“Tukiwa kwenye kikao, baba (mkwe, Yahaya Nguku) alijaribu kuzungumza kwa njia simu na mtoto wake (mume wake), lakini majibu aliyomjibu baba yalikuwa ni ya karaha,” alisema na kwamba akaamua kurudi Mbalizi kumsaka.

Alisema Ijumaa, walimuona mumewe akiwa na viongozi wa Serikali na ndipo walipoambiwa kwamba mume wake amesema ameona sehemu mtoto wake alipofukiwa na hivyo wakaamua kwenda.

Alisema walipofika eneo hilo, mumewe akafukua na kukuta mguu wa mtoto huyo ukiwa umeviuringishwa kwenye mfuko wa plastiki.

“Mguu wenyewe ulikuwa unaonekana unyayo tu kwa chini, vidole vimekatwa na ulikuwa umevunda,” alisema.

“Lakini tuliona ujasiri wa ajabu kwa mume wangu. Aliushika hivi na kuurusharusha huku akisema huu nina uhakika ni mguu wa mtoto wangu.”

Alipoulizwa ana uhakika gani, alijibu tena kuwa ana uhakika, ndipo viongozi walipopiga simu kwa diwani wa eneo husika na alipoendelea kusisitiza kuwa ni mguu wa mwanae, aliwekwa chini ya ulinzi hadi polisi walipofika na kuondoka na watu wote.

Alisema baada ya kuhojiwa kituoni, polisi wakaondoka na mumewe kwenda kumkamata mfanyabiashara huyo.

“Waliporudi, tukaondoka kwenda eneo ambako walimtupa mwanangu (milima ya Igurusi-Mbarali). Tulikuta shimo refu sana, lakini mimi hawakuniruhusu kuingia,” alisema.

Alisema waliambatana na vijana ambao ni wajukuu wa baba mkwe ambao waliingia kwenye shimo na kutambua maiti kuwa ni ya Rose na kutoka nayo.

Babu wa Rose alisema awali taarifa za kupotea kwa mjukuu wake alizipata, lakini hakutilia uzito akiamini kuwa angeambiwa rasmi. Alisema baadaye mtoto wake alimueleza kuwa mjukuu amepotea alipoenda wakati akiwa hotelini Mbeya alikoenda naye naye kutafuta maisha.

Alisema aliamua kwenda naye kwa kuwa angemuacha angeweza kupotea kwa kuwa alikuwa bado anasoma chekechea.

Alisema majibu hayo hayakumridhisha, hivyo alimtaka kijana wake ampelekee babu yake Igurusi.

“Niliposema hivyo, yeye akanijibu kwa ukali akisema ‘una uchungu na mtoto wewe au mimi nina uchungu mwenye mtoto?’” alisema.

Alisema wakati akiendelea kutafakari maneno ya mtoto huyo, akasikia taarifa kuwa amekamatwa akiwa na mguu wa mtoto na baadaye wakaupata mwili.

Kaka wa mtuhumiwa huyo, Award Yahaha alisema walishaanza kuchimba kaburi la kuzika mwili, lakini polisi wamewazuia wakisema hadi uchunguzi ukamilike.

Chanzo: mwananchi.co.tz