Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, amesema, Wizara imeshirikiana na wadau kuandaa Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Ukeketaji.
Dk. Gwajima ameyasema hayo wakati akiwasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 bungeni mjini Dodoma leo.
Waziri huyo amesema mkakati huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2020/21 – 2024/25, ili kuhakikisha kwamba vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike na wanawake vinatokomezwa.
Mkakati huo unalenga kupunguza ukeketaji nchini kutoka asilimia 10 mwaka 2015/16 hadi asilimia 5 mwaka 2021/22 na hatimaye kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka 2024/25.