Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane wa nyama ya swala aachiwa huru

Mjane Nyama Ya Swala Mjane wa nyama ya swala aachiwa huru

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa, Elvin Mgeta amemuachia huru Maria Ngoda ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kosa la kukutwa na vipande 22 vya nyama ya swala.

Kwa kupitia uamuzi wa mahakama hiyo, Jaji Mgeta amesema kutokana na hoja zilizowasilishwa na mkata rufani Ngoda hana hatia na yupo huru.

Amesema rufaa hiyo iliyosimamiwa na Mawakili wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa ilikuwa na hoja 13 zilizoonesha mashtaka yaliyotolewa dhidi ya Ngoda hayakuthibitishwa na mahakama iliyotoa hukumu hiyo.

Maria alihukumiwa miaka 22 jela, Novemba 3, 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Said Mkasiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live