Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjamzito ajichana tumbo, amtoa mtoto

60936 Mama+pic

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sumbawanga. Mwanamke mmoja aitwaye Joyce Kalinda anayedaiwa kujichana tumbo na kitu chenye ncha kali na kutoa mtoto akiwa hai amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa na kulazwa kwenye wodi ya wagonjwa wanahitaji uangalizi wa karibu (ICU)

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk John Lawi alisema kuwa mgonjwa amefikishwa hospitalini hapo tangu juzi na anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa wataalamu wa afya wa hospitali hiyo.

Dk Lawi alisema hali ya mwanamke huyo na mtoto wake inaendelea vizuri ila wamempunzisha katika wodi hiyo ili aweze kupata utulivu baada ya kupata matibabu katika kituo cha kirando wilayani Nkasi.

“Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa kwa kuwa tumeandaa utaratibu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kupitia kwa mganga mkuu wa mkoa, mtapata taarifa zote mnazozitaka kuhusu mgonjwa huyo,” alisema Dk Lawi.

Inadaiwa kuwa juzi saa 11 alfajiri mwanamke huyo alipelekwa katika kituo cha afya Kirando akiwa amepasuka sehemu ya tumbo na watu aliokuwa nao wakiwa wamebeba mtoto.

Chanzo: mwananchi.co.tz