Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misokoto 5000 ya Bangi yanaswa

Bangi 1 Kamanda Musilim ameonya kuhusu matendo ya uhalifu mkoani humo

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi.

Katika msako ulifanywa na jeshi la polisi kwa nyakati tofauti Manispaa ya Morogoro lilifanikiwa kukamata misokoto 5,000 sawa na kilogramu 25 ya bangi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim akizungumza na waandishi wa habari amesema tukio la kwanza lilitokea Mei 13, 2022 katik kata ya Lukobe ambapo askari wakiwa doria walimkamata Paulo Gaitano (24) mkulima na mkazi wa Mafiga.

Muslim alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa na mkisokoto 5,000 ya bangi akiwa amehifadhi kwenye boksi kwa kuifunika na lailoni nyeusi, huku akiwa ameifunga kwenye pikipiki aina ya Haojue rangi nyeusi.

Tukio la pili kamanda huyo alisema lilitokea Mei 22, 2022 maeneo ya Msamvu shule, kata ya Mwembesongo ambapo alikamatwa Selina Emilia (50) mkazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa na bangi viroba viwili sawa na kilogramu 40.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live