Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mirungi kilo 214 yampandisha kortini

Wed, 16 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Arusha nchini Tanzania, Taqabbal Mwasha amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi yenye uzito wa kilo 214.69.

Wakili wa Serikali, Nasua Candid amedai leo Jumanne Oktoba 15, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kuwa mshtakiwa huyo ana kabiliwa na kosa moja la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Amedai Septemba 5, 2019 katika ofisi ya Posta makao makuu mshtakiwa huyo alikutwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi yenye uzito wa gramu 214.69.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mwaikambo ameahitidha shauri Hilo hadi Oktoba 28, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz