Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mimba ya mwanafunzi yampeleka jela miaka 30

88162 Mimba+pic Mimba ya mwanafunzi yampeleka jela miaka 30

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Misungwi. Mkazi wa kitongoji cha Isagehe wilayani hapa mkoa wa Mwanza, Juma Masalu (20) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa makosa ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu Eric Marley baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa alitendo makosa hayo.

“Ushahidi wa shahidi wa pili upande wa mashtaka haupingiki kuwa ulimbaka kwani aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa anamfahamu alifanya naye mapenzi kwenye kichaka na hajawahi kushiriki na wengi zaidi yake” alisema.

Mahakama baada ya kupitia ushahidi huo na wa mshtakiwa, ilimtia hatiani na kumtaka ajitetee ili apunguziwe adhabu.

Mshtakiwa alidai hakutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama imsamehe.

Hata hivyo, Mahakama ilitupuuza utetezi huo na kumhukumu kosa la kubaka kwenda jela miaka 30 na kumpa mimba mwanafunzi adhabu hiyo hiyo, lakini kwa sababu adhabu zinafuatana atatumikia miaka 30.

Awali, mwendesha mashtaka wa polisi, Ramsoney Salehe akimsomea hati ya mashtaka alidai kati ya Oktoba 2018 na Julai mwaka huu, kijiji cha Isakamawe Masalu alifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza Sekondari ya Isakamawe mwenye miaka 17 na kusababishia ujauzito kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 130 na 131 (1) 2 (e) sura ya 16.

kama ilivyorejewa mwaka 2002 na sheria ya Elimu kifungu cha 60(4) kifungu kidogo (4) cha sheria ya Elimu sura 353 kama ilivyorejewa na sheria ya 2 ya mwaka 2016.

Chanzo: mwananchi.co.tz