Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miguu ya nyumbu yampeleka jela miaka 20

24810 Pic+nyumbu TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Marwa Kisiri (19), mkazi wa kijiji cha Tamukeri wilayani hapa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na miguu miwili wa nyumbu yenye thamani ya Sh1.4milioni.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya  ya Serengeti, Ismael Ngaile katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 98/2018, amesema mshtakiwa atatumikia kifungo hicho baada ya kutiwa hatiani.

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Emmanuel Zumba amesema mshtakiwa alikamatwa Agosti 18, 2017 katika korongo la Tamukeri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Chanzo: mwananchi.co.tz