Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mifuko ya plastiki yawafikisha kortini wafanyakazi TBS, raia wa China

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyakazi wawili wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na rai mmoja wa china wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo kuingiza mifuko ya plastiki isiyokuwa na viwango.

Washtakiwa hao wamefikishwa leo Jumatano Septemba 4, 2019 na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo.

Wakili wa Serikali, Janeth Magoha amewataja washtakiwa hao kuwa niĀ  Zuopo Wang, Wasalim Msilamdunda na Aman Mollel.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili Magoha amedai washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kula njama na kutenda kosa kinyume na sheria.

Amedai katika tarehe isiyofahamika wala mahali ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam washtakiwa hao walikula njama na kuingiza mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango.

Katika shtaka la pili, amedai mshtakiwa Wasalim na Amani wanadaiwa kati ya Agosti 2 na 8, 2019 wakiwa ni watumishi wa umma waliandaa na kusaidia kutendeka kwa kosa la jinai kwa kuruhusu mifuko ya plastiki yenye dhamani ya Sh73 milioni ambayo haijaidhinishwa na TBS.

Pia Soma

Advertisement
Katika shtaka la tatu washtakiwa hao wanadaiwa kusaidia kutendeka kwa kosa la jinaiĀ  ambapo amedai kati ya Agosti 2 na Agosti 8,2019 wakiwa Wilaya ya Ilala wakiwa sio watumishi wa umma walishirikiana na watumishi wa umma kuiingiza mifuko ya plastiki yenye dhamani ya Sh73 mlioni.

Katika shtaka la nne, washtakiwa hao wanadaiwa kuingiza mali kwenye masoko ambapo ni kinyume na sheria za Tanzania

Wakili Magoha amedai washtakia hao wakiwa Mbezi Makonde walikutwa na maofisa kutoka TBS, Baraza la Usimamizi wa Mazingira (Nemc) waliingiza marobota 255 ya mifuko ya plastiki isiyokidhi vigezo vya shirika la viwango.

Katika shtaka jingine, washtakiwa Wasalim Msilamdunda na Aman Mollel wakiwa waajiriwa wanadaiwa kutumia mamlaka yao vibaya.

Inadaiwa kati ya Agosti 2 na 6, 2019 wakiwa maofisa walioajiriwa na TBS walishindwa kuwajibika na kuruhusu kuingiza kwa marobota 255 ya mifuko ya plastiki isiyokuwa na viwango.

Wakili Magoha amedai upelelezi wa kesi huyo haujakamilika nakuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Hassan Kiangio amedai upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati ili kesi hiyo ianze kusikilizwa kwa wakati kwakuwa kesi inayowakabili haina dhamana.

Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi huyo hadi Septemba 17, 2019 kwaajili ya kutajwa na washtakiwa wote wamepelekwa rumande kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz