Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mifugo 400 ya magendo yakamatwa Tanga

Mifugo DPP Mifugo 400 ya magendo yakamatwa Tanga

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi limefanikiwa kukamata jumla ya mifugo 400, ambayo ilikua inasafirishwa kwenda Nje ya Nchi bila kufuata utaratibu.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua leo Oktoba 28, 2023 amebainisha kuwa mifugo hiyo imekamatwa katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga kupitia doria ambayo bado inaendelea na ilikua inatoroshwa kwenda nchi jirani kwa njia za magendo.

Sambamba na hilo pia amesema kuwa katika kuhakikisha wafugaji na wafanyabiashara wanafuata taratibu, kwa mwezi Oktoba mwaka huu Jeshi hilo limefanikiwa kutoa elimu kwa wafugaji katika minada mbalimbali nchini ambapo hadi kufikia Oktoba 28 jumla ya vipindi 149 vya elimu vimetolewa kote nchini.

ACP Pasua amefafanua kuwa kupitia elimu ambayo wanaendelea kuitoa imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya wizi wa mifugo sambamba na migogoro ya wakulima na wafugaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live