Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miezi 33 diwani yupo mahabusu kwa tuhuma za mauaji

82522 Pic+diwani Miezi 33 diwani yupo mahabusu kwa tuhuma za mauaji

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Imetimia miezi 33 ambayo, diwani wa Zanka halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani hapa, Lista Chilangwa akiwa mahabusu kutokana na deni la Sh12 milioni.

Hata hivyo, halmashauri hiyo imeendelea kulipa deni hilo analodaiwa na benki ya CRDB alilokopa 2016 miezi michache baada ya kuchaguliwa.

Chilangwa yupo mahabusu kwa tuhuma za mauaji ya Isaya Bayanga (60) wa kijiji cha Mkondahi, ambaye (Bayanga) alikuwa akimdai Sh4 milioni hali iliyosababisha kuingia katika mgogoro mkubwa.

Agosti mwaka jana, Mwananchi liliibua sakata la mwanasiasa huyo kuendelea kulipwa posho ya kila mwezi hadi wakati huo zilikuwa zimetumika zaidi ya Sh7 milioni, huku uongozi ukidai wangeendelea kumlipa kwani bado ni mtuhumiwa.

Hata hivyo, mkurugenzi wa wilaya hiyo Dk Fatuma Mganga alisema jana kuwa walisitisha malipo ya kila mwezi badala yake, wamebeba jukumu la deni alilokuwa amekopa.

Dk Mganga alisema isingekuwa rahisi kuendelea kumlipa posho wakati ahudhurii vikao vina yotambulika kwa mujibu wa sheria. “Mimi ni mgeni hivyo sina uhakika alikopa shilingi ngapi lakini tunaendelea kulipa kwa sababu tulimdhamini, hayo mengine muulize mwenyekiti,” alisema. Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Danfod Chisomi alikiri wanaendelea kulipa deni hilo hadi litakapomalizika lakini posho walisitisha.

Chanzo: mwananchi.co.tz