Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka 60 jela kwa kumbaka, kumpa mimba mwanafunzi

UBAKAJI SERIKALI.webp Miaka 60 jela kwa kumbaka, kumpa mimba mwanafunzi

Mon, 18 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Wilaya ya Singida, imemhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha jumla ya miaka 60 jela mkazi wa Kijiji cha Mpipiti, Kata ya Mudida, Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Abduli Bakari (27), baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Elizabeth Barabara, alidai kwamba katika siku siku isiyojulikana Februari, mwaka jana, mshitakiwa alimbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mudida.

Mwendesha Mashtaka huyo alidai pia kwamba huku akijua kwamba binti huyo ni mwanafunzi, mshitakiwa amekuwa akimlaghai mwanafunzi huyo kwa kumpa fedha pamoja na kumnunulia mahitaji mbalimbali ili kumshawishi kufanyanaye tendo la ndoa.

Hata hivyo, baada ya kusomewa shitaka hilo mshitakiwa alikana na ndipo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano mahakamani, ambao walitoa ushahidi ulioithibitishia mahakama hiyo bila kuacha shaka yoyote kwamba mshitakiwa ndiye aliyembaka mwanafunzi huyo.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka huyo kuwa katika siku isiyojulikana Februari, mwaka jana mshitakiwa huyo alimpa mimba mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 15.

Barabara alidai pia kwamba huku akijua kwamba binti huyo ni mwanafunzi, alimpa mimba.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, mshtakiwa alikana lakini mashahidi watano walitoa ushahidi uliothibitishia mahakama bila kutia kuacha shaka yoyote kwamba mshitakiwa ndiye aliyempa mimba mwanafunzi huyo.

Kabla ya kutoa hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 230/2019, Hakimu Mfawidhi, Robert Oguda, alisema matukio ya vitendo vya ubakaji na mimba katika wilaya ya Singida vimekithiri sana, hali inayochangia mabinti wadogo kupoteza masomo yao bila sababu zozote za msingi.

Akitoa hukumu hiyo, Oguda alisema kwamba ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya mshtakiwa huyo, anamhukumu mshitakiwa kwenda kutumikia adhabu ya miaka 30 jela kwa kosa la kwanza la kubaka na katika shitaka la pili la kumpa mimba, alimhukumu pia kifungo cha miaka 30 jela, na makosa yote yanaenda kwa pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live