Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka 4 Jela kwa kumkata kiganja bosi wake

Jela Miaka 4 Miaka 4 Jela kwa kumkata kiganja bosi wake

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka minne jela Baraka Luoga (20) mkazi wa Kimelembe wilayani humo kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata kiganja cha mkono bosi wake kwa madai ya sh. 65,000.

Tukio hilo ambalo lilitokea Desemba 25, 2022 ambapo mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo wakiwa mashambani baada ya kupishana kauli na bosi wake huyo wakati wakieleweshana juu ya malipo ya pesa hizo.

Baada ya kusomewa shitaka lake kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo na mwendesha mashtaka Angelo Marco mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa mahaka ya wilaya Ludewa Isaac Ayengo mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa hilo.

Aidha mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa kifungu cha sheria ili iwe fundisho kwa wengine hivyo hakimu Ayengo akatoa hukumu ya kifungo cha miaka 4 jela kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 225 sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Hata hivyo mshitakiwa huyo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ni kosa lake la kwanza na ana wazazi walio wazee wanao mtegemea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live