Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka 30 jela kwa kumpa mimba mwanafunzi kidato cha nne

71821 Mimba+pic

Sat, 17 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kigoma imemuhukumu miaka 30 jela mkazi wa kata ya Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji, Isack Balayabala (25)  baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Kaulananga.

Akisoma hukumu hiyo leo Ijumaa Agosti 16, 2019  hakimu wa mahakama hiyo, Eliya Baha amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 2018 kwa  kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.

Katika kesi hiyo ya  jinai namba 46 ya mwaka 2019 mahakama hiyo imesema  imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 60A kifungu kidogo cha (3) cha sheria ya elimu namba 353 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 kuwa mtu yeyote atakayempa mwanafunzi ujauzito atakuwa amevunja sheria na atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.”

“Kutokana na ushahidi wa upande wa mlalamikaji uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano akiwepo aliyepewa ujauzito, baba wa mwanafunzi huyo, mwalimu mkuu katika shule aliyokuwa akisoma ,askari wa upelelezi na daktari wa  hospitali aliyempima mahakama haina shaka na ushahidi huo, "amesema hakimu Baha.

Awali wakili wa Serikali, Happy Mayunga aliitaka mahakama hiyo kutoa adhabu kali kama fundisho kwa wanaokatisha ndoto za elimu kwa wanafunzi wa kike kwa kuwapa mimba.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz