Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka 10 jela kwa kumfanyia ukatili mtoto wa miaka minne

Ukatili Pc Data Ahukumiwa miaka 10 Jela

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemuhukumu, Eva Timotheo (27) kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kosa la kumfanyia ukatili wa kingono mtoto wa kike wa miaka minne.

Awali mwendesha mashitaka wa Polisi Wilaya ya Igunga, Alex Kataya, aliiambia mahakama mbele ya hakimu wa wilaya ya Igunga, Godfrey Rwekiti kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 19, 2020.

Amesema katika tarehe hiyo, mshitakiwa huyo alimfanyia kitendo cha ukatili wa kingono mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kumuingizia kitu butu kwenye sehemu zake za siri na kumsababishia maumivu makali.

Kataya ameendelea kuiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 138 C (1) (2) (b) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Baada ya kusomewa shitaka lake mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na ndipo upande wa mashitaka ulipopeleka mashahidi sita mahakamani akiwemo mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo ambapo mashahidi wote walimtambua mshitakiwa.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili hakimu Rwekiti alisema pasipo shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka umemuona mshitakiwa ana hatia hivyo mahakama inamuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 10 gerezani.

Chanzo: Mwananchi