Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhitimu darasa la saba akutwa amekufa nyumbani kwa mfanyabiashara

31689 KIFOPIC Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi

Fri, 14 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Mhitimu wa darasa la saba Shule ya Msingi Kashai, Fredrick Florian (13) amekutwa amekufa huku mwili wake ukining'inia kwenye geti la ghala la mfanyabiashara anayeuza vipuri vya magari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema hayo leo Ijumaa Desemba 14, 2018 na kwamba wanamshikilia Kanzari Ronard (46) kwa uchunguzi kwa kuwa ndiye anayetumia ghala hilo kuhifadhi vipuri.

Amesema wamebaini tukio hilo juzi katika mtaa wa Majengo mjini Bukoba, akibainisha kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kinatia shaka kwa kuwa mfanyabiashara huyo alikuwapo eneo hilo la tukio saa moja kabla ya mwili wa kijana huyo kuonekana.

Malimi amesema mwili wa Florian ulikutwa unaning'inia kwenye nondo zenye ncha kali za geti la ghala hilo na kuwa eneo hilo ni makazi ya watu na siyo mbali na nyumbani kwa wazazi wa mwanafunzi huyo.

Amesema eneo la tukio ni miongoni mwa maeneo yaliyotumiwa na mwanafunzi huyo kucheza na wenzake na kwamba, wazazi wake tayari wamejitokeza wanasubiri taratibu za uchunguzi zikamilike ili waruhusiwe kufanya mazishi.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz