Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhasibu Wizara ya Mambo ya Ndani atupwa jela miaka miwili

Hukumu Pc Data Mhasibu Wizara ya Mambo ya Ndani ahukumiwa jela miaka miwili

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Mhasibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini, Christina Kaale kulipa faini ya Sh8 milioni au kwenda jela miaka miwili, baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa Sh15.2 milioni mali ya wizara hiyo.

Kaale anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga wafanyakazi wastaafu wa wizara hiyo.

Pamoja na adhabu hiyo, mahakama pia imemtaka Christina kuilipa fidia Wizara hiyo ya Sh15.2 milioni anazodaiwa kufanya ubadhirifu, mara atakapomaliza kutumikia adhabu kifungo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Julai 29, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live