Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhasibu Wizara ya Afya kizimbani kwa ubadhirifu wa Sh31 milioni

15803 PIC+TAJKUKURU TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita imemfikisha mahakamani mhasibu wa wizara ya afya kwa makosa ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri na ubadhirifu wa Sh31 milioni.

Mshtakiwa huyo Nelly Mwalukuta ambaye ni mtumishi wa wizara ya afya alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani Geita Septemba 04, 2018

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Jovith Kato, mwendesha mashtaka wa Takukuru, Denis Lekayo alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2014 na Novemba 30, 2014.

Mshtakiwa andaiwa kutenda kosa katika ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Geita akiwa ni mhasibu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Lekayo aliieleza Mahakama kwamba kwa makusudi mshtakiwa alitumia ankara namba 23028 ya Oktoba 10, 2014 kumlaghai mwajiri wake kwa kuonyesha lita 13,191.51 za mafuta zenye thamani ya zaidi ya Sh31 milion zilinunuliwa na ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Geita kutoka kituo cha kuuza mafuta cha Nsagali.

Baada ya kufanya udanganyifu huo, mshtakiwa andaiwa kufuja fedha hizo kwa matumizi yake binafsi.

Mshtakiwa alikana kosa dhidi yake na kupelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Serikali na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani isiyopungua Sh15 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz