Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga wa jadi kortini kwa kunajisi wanafunzi

4fa419169f6b9b0631d827b4da28cb65 Mganga wa jadi kortini kwa kunajisi wanafunzi

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGANGA wa jadi, Saidi Omari (38), mkazi wa mtaa wa Zahanati, kata ya Mafi ga, Manispaa ya Morogoro amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro akikabiliwa na mashitaka matatu ya kunajisi watoto watatu wa kiume ambao ni wanafunzi wenye umri wa miaka tisa.

Mwendesha mashitaka wa serikali, Tumaini Mafulu, akimsomea mashitaka juzi mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Elia Mrema.

Alidai Omari anakabiliwa na mashtaka matatu ya ulawiti ambayo ni kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu namba 154 kifungu kidogo cha kwanza (a).

Mwendesha mashtaka wa serikali alidai Julai Mosi huu mpaka Septemba 9, mwaka huu, anasadikika kutenda kosa la kuwaingilia kinyume na maumbile watoto watatu wa kiume wenye umri wa miaka tisa wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

Mshitakiwa alikana kutenda makosa hayo na hakimu aliahirisha kesi hadi Oktoba 15, mwaka huu itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande.

Chanzo: habarileo.co.tz