Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga mbaroni kwa kumbaka mwanamke mfanyabishara wa madini

Kamanda All Makame Hamad Mganga mbaroni kwa kumbaka mwanamke mfanyabishara wa madini

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: Malunde

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mwanaume aitwaye Simbuka Makande (62) mganga wa kienyeji mkazi wa Kijiji cha Magengase Mkoa wa Tabora kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mfanyabiashara wa madini ya dhahabu (32) Mkazi wa Kijiji cha Katuma Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi baada ya kumrubuni kuwa atamsafishia nyota yake apate mali nyingi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi All Makame Hamad amewaambia waandishi wa habari kuwa mganga huyo wa Kienyeji alikuwa ametokea Mkoani Tabora na kufikia katika Kijiji hicho cha Katuma na kukodi chumba kwenye nyumba ya kulala wageni.

"Mwanamke huyo naye alikuwa amefikia kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni huku akiwa anaendelea kufanya shughuli za biashara yake ya madini ya dhahabu yanayochimbwa kwenye Kijiji hicho cha Katuma ndipo mwanamke huyo alipokutana na mganga huyo ambapo mganga alimweleza mwanamke huyo kuwa anao uwezo wa kuwasafishia watu nyota zao ili waweze kupata mafanikio kwenye shughuli zao na moja ya masharti yake ni kufanya naye mapenzi,"ameeleza.

Amesema ndipo mganga huyo alimrubuni mwanamke huyo na kufanya naye mapenzi kwa nyakati tofauti tofauti na pia mhanga aliweza kumpatia mganga kiasi cha shilingi milioni moja na elfu sitini.

Amebainisha kuwa mganga huyo pia anatuhumiwa kufanya vitendo hivyo kwa watu watatu Mkoani Katavi na kujichukulia kwa watu hao kiasi cha shilingi milioni nne na laki sita.

"Amekuwa akiwatapeli watu hao kuwa ameshawasaidia viongozi wengi kupata mafanikio na kisha kufanya nao mapenzi kwa kuwarubuni kuwa atawasaidia kupata mafanikio kama hayo katika biashara zao na maisha kwa ujumla",amebainisha.

Kamanda Makame amesema mtuhumiwa amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na jeshi la Polisi na mara upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chanzo: Malunde