Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga jela miaka 30 kubaka mke wa rafiki

Jela 1?fit=660%2C330&ssl=1 Mganga jela miaka 30 kubaka mke wa rafiki

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

MAHAKAMA ya Mkoa B Chakechake imemuhukumu mganga wa kienyeji kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mke wa rafiki yake.

Sambamba na kifungo hicho, mahakama imemwamuru kumlipa mwathirika fidia ya Sh. milioni moja.

Mganga huyo, Issa Abdalla Haji (41) mkazi wa Wawi Wilaya ya Chakechake, amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukubali kosa hilo.

Akisomewa shtaka na Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ali Amour Makame, mshtakiwa alikubali kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama impunguzie adhabu.

“Mshtakiwa ulimbaka mwanamke baada ya kumwaminisha kwamba wewe ni mganga wa kienyeji utakayemfanyia dawa ya kumtoa mume wake ambaye yuko rumande anayeshtakiwa katika kesi ya jinai namba 140/2021, kosa la wizi wa kutumia silaha, jambo ambalo ni kosa kisheria,” alidai mwendesha mashtaka kisha mshtakiwa kukubali kosa.

Hakimu Luciano Nyengo, baada ya mshtakiwa kukubali kosa, alimwamuru kwenda chuo cha mafunzo (jela)  miaka 30 na kumlipa mwathiriwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya hakimu huyo, mshtakiwa alikuwa rumande na rafiki yake, ikiwa yeye anakabiliwa na tuhuma za wizi huku rafiki yake akikabiliwa na tuhuma za wizi wa kutumia silaha.

“Walipokuwa rumande rafiki yake alimwambia amwambie mke wake akamchukulie dhamana ili na yeye akitoka akamwambie mke wake akamchukulie dhamana,” alisema hakimu.

Alisema baada ya mganga huyo kupata dhamana, alikwenda moja kwa moja kwa mke wa rafiki yake na kumwambia akamchukulie mumewe dhamana huku akimpa masharti ya uganga.

“Alimwambia ili mume wako apewe dhamana, lete nywele za sehemu za siri za mbele pamoja na mbegu za kiume, akimaanisha wafanye mapenzi ili wapate hizo mbegu za kiume,” alisema Hakimu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 11, mwaka huu, saa 12:00 jioni Wawi, Chakechake, kwa kumbaka mwanamke huyo bila ridhaa baada ya kumwaminisha kwamba atamfanyia dawa ya kumtoa mume wake rumande.

Kufanya hivyo, kwa mujibu wa hati ya mashtaka, ni kosa kinyume na kifungu cha 108 (1), (3),(d), na 109(1) cha Sheria ya Adhabu, Nambari 6 ya mwaka 2018, Sheria ya Zanzibar.

Chanzo: ippmedia.com