Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga aliyeipa sumu familia nzima kuchunguzwa

Muliro J Muliro Mganga aliyeipa sumu familia nzima kuchunguzwa

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: eatv.tv

Jeshi  la Polisi Kanda maalum  ya Dar es Salaam  linachunguza  tukio la mtu mmoja aliyejifanya Mganga wa jadi maeneo ya Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es Salaam na kuwanyeshwa Dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu  na kuwaibia watu  16 wa wafamilia moja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamishina wa kanda Maalum CP Muliro Jumanne Muliro amesema  tukio hilo lilitokea Februari 18 Mwaka huu majira ya Saa tatu usiku wakati mtu huyo aliyejifanya Mganga wa wajadi na kuingia nyumbani kwa familia ya  Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibia  mke wake Fatuma Abdallah (52) aliyekuwa  anasumbuliwa na tatizo la miguu.

“Aliwanywesha  Dawa  iliyowalewesha familia nzima  wakapoteza fahamu na kuwaibia simu tano za mkononi  na kuondoka" amesema Kamishina Muliro

Kamishina Muliro ameongeza  kuwa kufuatia  tukio hilo jeshi limetoa onyo kwa wanaojifanya waganga wakienyeji  kuwa halitosita kuwachukulia hatua.

Katika hatua Nyingine Jeshi hilo limewataka Mamlaka  husika inayohusika  Sukari kuuza kwa bei elekezi na hatosita kuwachukulia hatua

Chanzo: eatv.tv