Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgambo wajeruhi wakidai Sh50,000, wadakwa na polisi

14936 Mgambo+pic TanzaniaWeb

Sat, 1 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam.  Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linawashikilia mgambo watatu wa manispaa ya Kinondoni kwa tuhuma za kumjeruhi mfanyabiashara, Robson Orotho mkazi wa Bunju.

Akizungumza na MCL Digital leo Ijumaa Agosti 31, 2018 Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Jumanne Murilo amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na kusambaa kwa taarifa zikiwaonyesha wakikiuka sheria za nchi.

Amesema mgambo hao walimshushia kipigo mfanyabiashara huyo kutokana na kushindwa kulipa Sh50,000 ya taka.

"Ni kweli tunawashikilia watuhumiwa watatu kwa kitendo walichokifanya, tumegundua ziko taratibu na sheria zilizokiukwa,” amesema.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Kelvin Edson, Gudluck Festo na Rehema Nyange ambao wote ni mgambo wa manispaa hiyo.

Kamanda Muliro ametoa wito kwa vyombo vyote vya Serikali na vile vya binafsi kufanya kazi kwa kufuata  misingi ya sheria, taratibu na kanuni za nchi .

Amebainisha kuwa tayari jalada la uchunguzi limefunguliwa na mfanyabiashara huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala na uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Siku za hivi karibuni zimesambaa picha za video katika mitandao ya kijamii zikionyesha mgambo wakitoa kipigo kwa watu na kuzua taharuki, wengi wakiwa ni wafanyabiashara ndogondogo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz