Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgambo maarufu Moshi auawa

Kifo Kifo Mauiaji.png Mgambo maarufu Moshi auawa

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgambo maarufu katika kata ya Bomambuzi Manipaa ya Moshi aliyekuwa pia dereva bajaji, Farjala Abdallah ameuawa na watu wasiojulikana, huku Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro likiahidi kuwasaka kwa udi na uvumba waliofanya mauaji hayo.

Mwili wa marehemu ulipatikana leo alfajiri ya Februari 21,2024 katika eneo la Uwanja wa Mandela ukiwa na majeraha, huku majirani wakifichua kile walichokisikia usiku wa manane kuwa marehemu alikuwa akijitetea kuwa sio mwizi.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi, Azizi Kalokola ,Diwani wa Kata ya Bomambuzi, Juma Raibu na mashuhuda mbalimbali wameelezea namna walivyopata taarifa za kuonekana kwa mwili wa dereva huyo leo alfajiri. Huku Diwani Raibu akiahidi kutoa kitita cha Sh500,000 kwa mtu atakayetoa taarifa fiche na sahihi zitakazosaidia kukamatwa kwa watu waliofanya mauaji hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live