Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyakazi atakiwa kuilipa TRC fidia ya Sh108,450

Mfanyakazi atakiwa kuilipa TRC fidia ya Sh108,450

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Xavier Kundi kulilipa shirika hilo fidia ya Sh108, 450 baada ya kukutwa na hatia ya wizi alipokuwa mtumishi wa umma.

Ametakiwa kulipa fidia hiyo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la wizi alipokuwa mtumishi wa TRC.

Mbali na adhabu hiyo, Mahakama hiyo imemhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha nje cha miezi sita kwa masharti ya kutojihusisha na makosa yoyote ya jinai ndani ya muda huo.

Akisoma hukumu hiyo leo Jumatano Desemba 11, 2019 Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally amesema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa huyo katika kosa la wizi baada ya kukiri.

Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo upande wa mashtaka ukiongozwa na mkurugenzi msaidizi wa mashtaka, Maternus Marandu umedai  mshtakiwa alimuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) kuomba kukiri shtaka na kusamehewa.

Marandu amedai kuwa mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka zaidi ya 14 yakiwemo ya kughushi tiketi za treni  lakini ametiwa hatiani katika shtaka moja la wizi akiwa mtumishi wa shirika hilo.

Marandu amedai miongoni mwa makubaliano waliyofanyikia baina ya mshtakiwa na DPP ni kumtaka mshtakiwa kulipa fidia ya Sh108,450.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 338/2018 mshtakiwa  anadaiwa kutenda kosa hilo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.

Mshtakiwa anadaiwa kati ya mwaka 2018 na 2019 katika mikoa hiyo alijipatia  kiasi cha Sh108,450 kwa njia ya wizi wakati akiwa mtumishi.

Chanzo: mwananchi.co.tz