Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara mwingine Tanzania aunganishwa kesi ya 'Papa Msofe'

91003 Pic+musofe Mfanyabiashara mwingine Tanzania aunganishwa kesi ya 'Papa Msofe'

Tue, 7 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar  es Salaam. Mfanyabiashara Emmanuel  Reuben (32), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kutatisha fedha kiasi cha Sh943 milioni.

Ruben mkazi wa Dar es Salaam amefikishwa mahakama hapo leo Jumatatu Januari 6, 2020 na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya.

Hata hiyo, Ruben ameunganishwa katika kesi ya uhujumu uchumi namba 124/2019 inayomkabili mfanyabiashara, Marijan Msofe maarufu 'Papaa Msofe na wenzake wanne.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni kula njama, kuratibu genge la uhalifu, kutakatisha fedha na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisomewa mashtaka yake, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya amedai mshtakiwa pamoja na wenzake wametenda makosa yao kwa nyakati tofauti tofauti.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, mshtakiwa anadaiwa  kutenda kosa hilo, kati ya Desemba 2018 na Septemba 2019, Jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa wakiwa na nia hiyo walijipatia dola za Kimarekani 300,000 (sawa na Sh.690milioni) kutoka kwa Pascal Camille, wakidai kuwa watamuuzia dhahabu kilo 200 ambayo wangemsafirishia kwenda Ureno wakati wakijua si kweli.

Pia anadaiwa katika kipindi hicho,  walimlaghai Johnson Mason kwamba watamuuzia kilo 20 za dhahabu yenye thamani ya Sh253 milioni na wangemsafirishia kwenda nchini Ureno wakati wakijua si kweli.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, Hakimu Issaya alisema mshtakiwa hatakiwi mujibu chochote Mahakamani hapo kutoka na Mahakamani ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa DPP.

Upande wa mashtaka walidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 13, 2020 itakapotajwa.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka kutakatisha fedha linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, mshtakiwa anadaiwa  kutenda kosa hilo, kati ya Desemba 2018 na Septemba 2019, Jiji la Dar es Salaam.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, Hakimu Issaya alisema mshtakiwa hatakiwi mujibu chochote Mahakamani hapo kutoka na Mahakamani ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa DPP.

Mbali na Ruben, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 124/2019 ni Marijan Msofe(53), maarufu kama 'Papa Msofe' wakili wa kujitegemea Mwesigwa Mhingo (36), Josephine Haule(38), Wenceslau Mtui (49) na Fadhil Mganga (61).

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao watano, walifikishwa Kisutu, Desemba 2, 2019 wakikabiliwa na mashtaka hayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz