Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara kortini kwa kusafirisha binadamu

Hukumu Pc Data Mfanyabiashara kortini kwa kusafirisha binadamu

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: mwanachidigital

Mfanyabiashara na mkazi wa Tabata Mawenzi, Mohamed Masoli (34) amefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, akikabiliwa na shtaka moja la usafirishaji haramu wa binadamu.

Masoli amefikishwa mahakamani leo, Oktoba 31, 2022 na kusomewa shitaka lake na wakili wa Serikali, Caroline Materu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.

Akimsomea hati ya mashtaka, wakili Materu amedai Masoli anakabiliwa na kesi ya jinai namba 168/2022 na alifanya kosa hilo Juni 11, 2021 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere( JNIA), akidaiwa kumsafirisha Rahma Yusuph kwa ahadi ya kumpatia ajira nje ya nchini. Also Read

Moto wazua taharuki Bukoba duka likiteketea Kitaifa 14 hours ago Wanaume washauriwa kupima saratani ya matiti Kitaifa 14 hours ago

Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka linalomkabili, alikana na upande wa mashtaka wamesema kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

"Mheshimiwa hakimu, kwa kuwa upelelezi umekamilika, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomewa hoja za awali (PH) mshtakiwa huyu," amesema wakili Materu.

Kwa upande wao mawakili wa mshtakiwa huyo, Douglas Mmari na Mohamed Majaliwa, waliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe ya karibu kwa kuwa mteja wao afya yake sio nzuri na amekaa Polisi kwa muda mrefu.

Hakimu Rugemalira baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, alimueleza mshtakiwa kuwa shtaka la kumsafirisha binadamu halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Baada ya maelezo hayo, hakimu Rugemalira aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14, 2022 itakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomea hoja za awali na Kisha kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka linalikukabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: mwanachidigital