Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara kortini akikabiliwa na mashtaka 106

Hukumu Pc Data Mfanyabiashara kortini akikabiliwa na mashtaka 106

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: mwanachidigital

Mfanyabiashara, Gaspton Danda (40) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 106 likiwamo la utakatishaji wa fedha zaidi Sh1.5 bilioni.

Wakili wa Serikali, Adolf Verandumi akishirikiana na wakili wa Serikali, Yusuph Aboud amedai mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 69 ya kugushi, mashtaka 36 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la utakatishaji wa fedha.

Verandumi akisoma hati ya mashata hayo alidai katika mshtaka hayo inadaiwa kuwa kati ya Agosti 26, 2020 hadi Novemba 10, 2020 maeneo benki ya CRDB Tawi la Msasani mshtakiwa huyo alighushi barua ya utambulisho na fomu ya kuombea mkopo ambapo alitumia akaunti za majina tofauti ya wafanyakazi 69 wa kampuni ya Savanna Mining.

Katika shtaka la kugushi inadaiwa kuwa kati ya Agosti 26, 2020 eneo la Benji ya CRDD Tawi la Msasani jijini Dear es Salaam mshtakiwa huyo aligushi barua ya Oktoba 26,2020 ikionyesha Jonson Clement bi mfanyakazi wa kampuni ya Savanna Mining.

Katika shtaka lingine mshtakiwa huyo aligushi fomu ya mkopo kiasi cha Sh49 milioni kwenye akaunti ya CRDB yenye jina la Jonson Clement huku akijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka lingine inadaiwa kati ya Oktoba 31, 2020 maeneo hayo mshtakiwa huyo alljipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh49 milioni kwenye akaunti ya CRDB yenye jina la Jonson Clement Hulu akijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka la mwisho la utakatishaji wa fedha inadaiwa kati ya Agosti 26, 2020 hadi Novemba 10, 2020 mshtakiwa huyo alijipatia zaidi ya Sh1.56 bilioni huku akijua ni zao ya makosa aliyoyafanya kujipatia kiasi hicho.

Chanzo: mwanachidigital