Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara apambana na majambazi kwa dakika 15 na kuwanyang'anya bunduki aina ya Shotgun

64679 MAJAMBAZI+PIC

Fri, 28 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Cassian Fortunatus (28) mkazi wa Kilosa amefanikiwa kumnyang’anya bunduki mmoja wa majambazi waliomvamia nyumbani kwake baada ya kurudi kwenye biashara zake.

Akisimulia tukio hilo Fortunatus alisema kuwa baada ya kufunga duka lake la huduma za kifedha akiwa na mke wake Zuhura Waziri walirudi nyumba na kabla ya kufika mlangoni ghafla walivamiwa na majambazi hao wawili ambapo mmoja aliyekuwa na bunduki aina ya ‘Shotgun Magnum’alifyatua risasi moja hewani na kuwaamuru waweke chini mkoba wenye pesa.

Alisema kuwa kwa hofu mke wake aliweka chini mkoba wake mdogo uliokuwa na fedha Sh 200,000 pamoja na simu mbili na yeye aliamua kugoma kuweka chini mkoba mkubwa uliokuwa na fedha alizotoka nazo dukani na ndipo majambazi hayo yalipofyatua risasi mbili hewani kwa lengo la kumtisha.

“Baadaye jambazi mmoja aliamua kuchukua ule mkoba wa mke wangu na kukimbia, nikabaki na jambazi mmoja nikipambana naye na wakati wote huo begi langu lenye hela nyingi likiwa mgomboni yule jambazi alipoona namzidi nguvu akakimbia ndipo nilipoanza kumkimbiza na kwa bahati nzuri alianguka chini na mimi nikamata nafasi nzuri ya kumkaba na kumnyang’anya ile bunduki ,” alieleza Cassian.

Alisema kuwa alipambana na majambazi hayo kwa dakika zisizozidi 15 na wakati wa mapambano hayo hakujua kama angefanikiwa kuwanyang’anya bunduki na fedha zake kuwa salama.

Hata hivyo alisema kuwa ujasili huo wa kupambana na majambazi aliupata kutokana na mazoezi anayofanya na kwamba miaka ya nyuma alikuwa akicheza mchezo wa karate.

Pia Soma

Kufuatia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbrod Mutafungwa pamoja na maafisa wa polisi wamemzawadia fedha taslimu Sh. 265,000 kwa kuonesha ukakamavu na ujasili uliofanikisha kupatikana kwa bunduki hiyo.

Akizunguzia tukio hilo kamanda Mutafungwa alisema kuwa amemzawadia kiasi hicho cha fedha kwa kuwa kazi aliyoifanya ilipaswa ifanywe na askari aliyepitia mafunzo lakini ujasili aliouonesha Cassian ni mfano wa kuigwa sio kwa watu wengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz