Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara anayedaiwa kuua kwa risasi kortini

MFANYABIASHARA KORTINI Mfanyabiashara anayedaiwa kuua kwa risasi kortini

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Kennedy Minja (47), mfanyabiashara maarufu wa Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro anayedaiwa kuua kwa kumfyatulia risasi mkazi wa Kilema, Deogratius Lyimo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi leo, Juni 6,2023.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Mei 17, 2023 katika barabara ya Himo-Marangu kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo, inaelezwa mfanyabiashara huyo aliendesha gari lake umbali wa kilomita 27 kutoka mji wa Himo hadi Moshi mjini ambako inadaiwa alijisalimisha kituo kikuu cha polisi.

Chanzo: Mwananchi