Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara akiri makosa, ahukumiwa kulipa Sh100 milioni

78208 Pic+hukumu

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, imemuhukumu Mfanyabiashara, Hilaly Akida kulipa Sh100 milioni baada ya kukiri mashtaka matatu likiwemo la kuwinda mnyama aina Twiga.

Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano Oktoba 2, 2019, Hakimu Vick Mwaikambo amesema kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa mshtakiwa huyo kufanya kosa, anajutia na amekiri kosa na fedha hizo zitapelekwa serikalini.

“Kwa kuwa mshtakiwa ni kosa lake la kwanza halafu ni msamaha uliotolewa na Rais John Magufuli, alitoa kwa watu walioshtakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi, hivyo mahakama hii inakupa adhabu ya kurudisha fedha kiasi cha Sh100 milioni,” amesema Vick.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka uliowakilishwa na wakili wa Serikali Mkuu, Rosemary Shio na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon ulidai kosa hilo ni la kwanza na mshtakiwa amekiri kutokana na Rais Magufuli kutangaza kwa wale watu watakaokiri makosa yao watapatiwa msamaha.

Wakili Shio alidai upande wa mashtaka wanaiomba mahakama hiyo itoe adhabu ya kulipa Sh100 milioni na kiasi hicho kitarejeshwa Serikalini.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Rosemary Shio aliomba washtakiwa hao wasipewe adhabu kali kwa sababu wamekiri na pia msamaha aliotoa Rais Magufuli kwa wale watakaokiri makosa yao na kurudisha fedha.

Pia Soma

Advertisement
Inadaiwa kati ya Julai Mosi 2019 na Agosti 30,2019 katika maeneo ya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa makusudi walipanga njama ya genge la kihalifu wakishiriki kuwinda mnyama aina ya Twiga mwenye thamani ya Sh34.5 milioni.

Katika shtaka lingine, Julai Mosi 2019 na Agosti 30,2019 katika maeneo ya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kwa makusudi waliwinda Twiga mwenye thamani ya Sh34.5 milioni bila ya kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.

Katika shtaka la tatu, washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa Julai Mosi 2019 na Agosti 30,2019 katika maeneo ya Mkoa wa Pwani na Dar es  Salaam, walitakatisha fedha kwa kujihusisha moja kwa moja na miamala iliyohusu kufanya uhalifu kwa mnyama aina ya Twiga mwenye thamani ya Sh34.5 milioni huku wakijua kumuua mnyama huyo ni kosa.

Mbali na Akida kukiri mashtaka hayo na kulipa faini, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Haidary Sharifu, Ofisa wanyamapori wilaya ya Kisarawe, Amani Kavishe, Mwita Mataro na Msaidizi wa ofisa wa wanyamapori wilaya ya Kisarawe, Lebeti Mollel ambao hawajakiri mashtaka yao.

Hakimu Mwaikambo alisema washtakiwa hao wataendelea na kesi hiyo na wamerudishwa rumande hadi Oktoba 16, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz